sw_tn/rom/02/intro.md

2.2 KiB

Warumi 02 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Sura hii inabadilisha wasikilizaji wake kutoka kwa Wakristo wa Kirumi na kuwa wale ambao "wanahukumu" watu wengine na hawaamini Yesu. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/judge]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/believe]])

"Kwa hiyo huwezi kamwe kujitetea"

Kifungu hiki kinatazama nyuma katika Sura ya 1. Kwa njia fulani, kwa kweli huhitimisha kile Sura ya 1 inafundisha. Kifungu hiki kinafafanua kwa nini kila mtu duniani lazima aabudu Mungu wa kweli.

Dhana maalum katika sura hii

"Wenye kuitii sheria"

Wale ambao wanajaribu kutii sheria hawatahesabiwa haki kwa kujaribu kuiitii. Wale ambao wanahesabiwa haki kwa kumwamini Yesu wanaonyesha kwamba imani yao ni ya kweli kwa kutii amri za Mungu. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/justice]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/lawofmoses]])

Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii

Maswali ya uhuishaji

Paulo anatumia maswali kadhaa ya uhuishaji katika sura hii. Inaonekana nia ya maswali haya ya uhuishaji ni kufanya msomaji kuona dhambi zake ili amtegemee Yesu. (See: [[rc:///ta/man/translate/figs-rquestion]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/guilt]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/faith]])

Hali ya Kufikiri

Katika muktadha, "atatoa uzima wa milele" katika mstari wa 7 ni tamko la kufikiri. Ikiwa mtu anaweza kuishi maisha kamilifu, angepata uzima wa milele kama tuzo. Lakini Yesu peke yake alikuwa na uwezo wa kuishi maisha kamilifu.

Paulo anatoa hali nyingine ya kufikiri katika mstari wa 17-29. Hapa anaelezea kuwa hata wale wanaojitahidi kufuata sheria ya Musa wana hatia ya kukiuka sheria. Kwa Kiingereza, hii inahusu wale wanaofuata "maandiko" ya sheria lakini hawawezi kufuata "roho" au kanuni za jumla za sheria. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-hypo)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Nyinyi mnaohukumu"

Wakati mwingine, hii inaweza kutafsiriwa kwa njia rahisi. Lakini inatafsiriwa kwa njia hii isiyo ya maana kwa sababu wakati Paulo akimaanisha "watu wanaohukumu" anasema pia kila mtu anahukumu. Inawezekana kutafsiri hii kama "wale wanaohukumu (na kila mtu anahukumu)."

<< | >>