sw_tn/rev/07/intro.md

30 lines
1.4 KiB
Markdown

# Ufunuo 07 Maelezo ya jumla
## Muundo na mpangilio
Wasomi wengi wanaamini kwamba nusu ya kwanza ya sura hii inahusu uamusho mkuu miongoni mwa Waisraeli ambapo watu 144,000 watakuja kumuamini Yesu. Nusu ya pili ya sura hii inatuelezea uamusho mkuu miongoni mwa watu wa Mataifa ambapo watu wasiohesabika watakuja kumuamini Yesu. (Tazama: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/believe]] na [[rc://*/ta/man/translate/writing-apocalypticwriting]])
Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 7:5-8, 15-17
## Dhana muhimu katika sura hii
### Kuabudu
Watu kwenye sura hii wanaitikia matukio haya kwa kutubu na kuabudu.Hiki ndicho kiitikio cha kweli cha habari iliyoko katika kitabu hiki.(Tazama: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/reveal]], [[rc://*/tw/dict/bible/kt/repent]] na [[rc://*/tw/dict/bible/kt/worship]])
### Dhiki kuu
Hiki ni kipindi ambacho watu wa duniani wataadhibiwa vikali na Mungu. Kuna kutoelewana kuhusu kipindi hiki lakini wasomi wengi wanaamini kwamba hiki ni kipindi cha nusu ya mwisho ya miaka saba ya dhiki kuu inayotabiriwa katika Ufunuo 4-19 na katika sehemu zinginezo za maandiko.
## Mifano muhimu ya usemi
### Mwanakondoo
Hii inaashiria Yesu.Katika sura hii, inaashiria pia cheo cha Yesu.(Tazama: [[rc://*/ta/man/translate/figs-explicit]])
## Links:
* __[Revelation 07:01 Notes](./01.md)__
__[<<](../06/intro.md) | [>>](../08/intro.md)__