sw_tn/rev/06/09.md

36 lines
1.2 KiB
Markdown

# muhuri wa tano
"muhuri unaofuata" au "muhuri namba tano"
# chini ya madhabahu
Hii inaweza kuwa "katika kitako cha madhabahu."
# wale waliokuwa wameuawa
Hii inaweza kutafsiriwa na kitenzi. "wale ambao wameuwawa na wengine"
# neno la Mungu na kutokana na ushuhuda
Maana zinazowezekana ni 1) ushuhuda ni ushahidi wa Mungu juu ya ukweli wa neno lake (kama inavyooneshwa kwenye UDB), au 2) ushuhuda ni ushahidi wa aliye amini juu ya ukweli wa neno la Mungu.
# walioushika
Kuamini neno la Mungu na ushuhuda wake vinazungumziwa kama vitu ambavyo vinaweza kushikwa mikononi. "ambavyo waliamini"
# ulipiza kisasi damu yetu
Neno damu hapa linaonesha vifo vyao. "adhibu waliotuuwa"
# hata itakapotimia ... ambao watauawa
Hii inaonesha kuwa Mungu ameshaamua kwamba kuna idadi ya watu ambayo watauwawa na adui zao.
# watumishi wenzao na ndugu zao wa kike na wa kiume
Hili ni kundi la watu linalofafanuliwa kwa njia mbili: kama watumishi na kaka na dada. "Kaka zao na dada zao wanaomtumikia Mungu pamoja nao" au "waumini wenzao wanaomtumikia Mungu pamoja nao"
# ndugu zao wa kiume na wa kike
Wakristo wanazungumziwa kuwa kama ndugu wa kiume na wa kike. "Wakristo wenzao" au "waumini wenzao"