sw_tn/psa/093/001.md

32 lines
1.0 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# amevikwa na adhama; Yahwe amemvika na kujifunga na nguvu
Mwandishi wa zaburi anazungumzia nguvu ya Yahwe na adhama yake kana kwamba vilikuwa vitu ambavyo Yahwe alivaa. "anawaonesha wote kuwa ni mfalme mwenye uwezo" au "adhama yake ipo kwa ajili ya kila mtu kuona, kama joho ambalo mfalme huvaa; kila kitu kumhusu Yahwe kinaonesha kuwa ana nguvu na yuko tayari kufanya kazi kubwa"
# adhama
uwezo wa mfalme na jinsi mfalme anavyotenda
# kujifunga
kufunga mshipi — ukanda wa ngozi au kitu kingine ambacho mtu huvaa kiunoni — kujianda kwa ajili ya kazi au mapambano
# Dunia imewekwa imara
Hii inaweza kuelezwa kwatika hali ya kutenda. "Umeiweka imara dunia"
# haiwezi kusogezwa
Hii inaweza kuelezwa kwatika hali ya kutenda. "hakuna atakaye isogeza"
# Kiti chako cha enzi kimewekwa tangu nyakati za kale
Hii inaweza kuelezwa kwatika hali ya kutenda. "Ulikiweka kiti chako cha enzi tangu nyakati za kale"
# wewe ni tangu milele
"ulikuwepo siku zote"