sw_tn/psa/092/012.md

24 lines
847 B
Markdown

# Wenye haki watastawi kama mtende
Maana zinazowezekana ni kwamba watu wenye haki watakuwa kama mtende wenye afya kwa sababu 1) watakuwa imara au 2) wataishi muda mrefu.
# wataota kama mti wa seda ya Lebanoni
Maana zinazowezekana no kwamba watu wenye haki watakuwa kama mti wa seda unaoota katika nchi ya Lebanoni kwa sababu 1) watakuwa imara au 2) watu watawaheshimu.
# Wamepandwa
"Yahwe amewapanda" au "Yahwe anawatunza kana kwamba ni miti aliyoipanda"
# katika nyumba ya Yahwe ... katika nyua za Mungu wetu
Mwandishi wa zaburi anawazungumzia watu wanaomwabudu Mungu kwa ukweli kana kwamba walikuwa miti inayoota katika nyumba ya Yahwe.
# wanastawi
Mwandishi wa zaburi anawazungumzia watu wenye haki kana kwamba ni miti yenye afya. "wanakua vizuri" au "wana nguvu sana"
# katika nyua za Mungu wetu
katika baraza la hekalu Yerusalemu.