sw_tn/psa/085/010.md

24 lines
1.2 KiB
Markdown

# Uaminifu wa agano na uaminifu umekutana pamoja
Maana zinazowezekana ni 1) Mungu atakuwa mwaminifu kwa sababu ya agano lake na atafanya alichoahidi au 2) Mungu atakuwa mwaminifu kwa sababu ya agano lake na watu wataitikia kwa kuwa waaminifu kwake. Vyovyote vile uaminifu unazungumziwa kana kwamba ni mtu anayeweza kukutana na mwenzake.
# umekutana pamoja ... zimepigana busu
Inawezekana kuwa mwandishi anazungumzia wakati wa mbele ambapo Mungu atawasababisha watu wake kufanikiwa tena. zitakutana pamoja ... zitapigana busu"
# haki na amani zimepigana busu
Maana zinaziwezekana ni 1) watu watafanya kilicho sawa na mungu atawasababisha watu kuishi kwa amani au 2) Mungu atafanya kilicho sawa na kuwasababisha watu kuishi katika amani. Vyovyote vile, haki na amani zinazungumziwa kana kwamba ni watu wanajipiga busu.
# zimepigana busu
Hii ni njia ya kawaida ya marafiki kusalimiana.
# Uaminifu unachomoza kutoka kwenye ardhi
Watu wa duniani kuwa waaminifu kwa Mungu inazungumziwa kana kwamba uaminifu ni mmea unaoota ardhini. "Hapa duniani, tutakuwa waaminifu kwa Mungu"
# haki inaangalia chini kutoka angani
Mwandishi anaelezea haki kama mtu anatazama chin kama Mungu afanyavyo. "Mungu atatuangalia kwa fadhila na kutupa ushinid"