sw_tn/psa/045/005.md

24 lines
1.2 KiB
Markdown

# watu wanaanguka chini yako
Msemo huu unamaanisha mfalme kuwashinda adui zake. Maana zinazowezekana ni 1) "watu wanaanguka miguuni mwako kwa kusalimu amri" au 2) "watu wanaanguka wakiwa wamekufa miguuni mwako."
# mishale yako iko mioyo ya adui wa mfalme
"mishale yako imechoma mioyo ya adui zako." Mwandishi anazungumza kwa mfalme huku akimweleza mfalme katika nafasi ya mtu wa tatu.
# Kiti chako cha enzi ... ni wa milele na milele
maneno "Kiti chako cha enzi" yanawakilisha ufalme na utawala wa mfalme. "Ufalme wako ... ni wa milele na milele" au "Utatawala ... milele na milele"
# Kiti chako cha enzi, Mungu
Maana zinazowezekana ni kwamba neno la "Mungu" 1) ni jina kwa ajili ya mfalme, ambaye ni mwakilishi wa Mungu au 2) linaboresha maneno "kiti cha enzi" na linamaanisha "Ufalme wako ambao Mungu amekupa"
# fimbo ya hukumu ni fimbo ya ufalme wako
Neno "fimbo" linawakilisha mamlaka ya mfalme kutawala ufalme wake. "unatawala ufalme wako kwa haki"
# Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta ya furaha
Mwandishi anazungumzia furaha kana kwamba ni mafuta ambayo Mungu alitumia kumtia mafuta mfalme. Mungu kumtia mafuta ni ishara inayowakilisha kwamba Mungu amemchagua kuwa mfalme. "Mungu alipokuchagua kama mfalme, alikufanya kuwa na furaha sana"