sw_tn/psa/023/001.md

28 lines
1.1 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Zaburi ya Daudi
Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.
# Yahwe ni mchungaji wangu
Mwandishi anamzungumzia Yahwe kana kwamba alikuwa mchungaji. Hii inasisitiza jinsi Mungu anavyowajali watu kama mchungaji anavyowajali kondoo wake. "Yahwe ni kama mchungaji kwangu" au " Yahwe ananijali kama mchungaji anavyojali kondoo wake"
# sitapungukiwa kitu
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nina kila kitu ninachohitaji"
# Ananifanya kulala chini kwenye malisho ya kijani
Mwandishi anajizungumzia kana kwamba ni kondoo, na anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni mchungaji. "Ananipa mapumziko kama mchungaji anavyowaongoza kondoo wake kulala chini kwenye malisho ya kijani"
# ananiongoza kando kando na maji yaliyotulia
Mwandishi anajizungumzia kana kwamba ni kondoo, na anamzungumzia Yahwe kana kwamba ni mchungaji. "ananipa ninachohitaji kama mchungaji anayewaongoza kondoo wake kando kando ya maji matulivu"
# maji yaliyotulia
"maji yanayotiririka taratibu." Maji haya ni salama kunywa.