sw_tn/psa/013/001.md

24 lines
853 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Kwa mwanamuziki mkuu
"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"
# Zaburi ya Daudi
Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.
# Hadi lini, Yahwe, utakuwa ukinisahau?
Swali hili linaulizwa kushika ufahamu wa msomaji na kuongeza msisitizo. Linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Yahwe, inaonekana kuwa umenisahau!
# Hadi lini ... uso wako kwangu?
Maneno "uso wako" yanaashiria Mungu kamili. Swali hili balagha linaulizwa kuongeza msisitizo. Linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Inaonekana unajificha kwangu!"
# Hadi lini adui yangu atashinda juu yangu?
Swali hili la balagha linaulizwa kuongeza msisitizo. Linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hakika adui zangu hawatanishinda daima!"