sw_tn/php/04/04.md

917 B

Muwe na furaha itokanayo na Bwana siku zote. Tena nasema muwe na furaha

Paulo anawaambia wakristo wa Filipi. Airudia amri ya kufurahi ili kuonyesha msisitizo wa umhimu wa kufurahia. "Furahini kwa sababu ya kile ambacho Bwana amefanya, tena nasema iweni na furaha"

Bwana amekaribia

Sentensi hii imetumika kulenga maana mbili ambazo ni: 1) Bwana Yesu Kristo yuko karibu na wakristo katika roho. 2) Siku ya Bwana Yesu kurudi duniani iko karibu

bali fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kuomba, kusali na kushukuru, mahitaji yenu yajulikane na Mungu

"mwambieni Mungu mahitaji yenu kwa kusali kushukuru"

Iliyo juu ya fahamu zote

"ile iliyozaidi ya uelewa wetu"

italinda mioyo na mawazo mawazo yenu

Hii inawakilisha amani ya Mungu kama askari alindaye hisia zetu na mawazo yetu kutoka kwenye hofu. "itakuwa kama askari na akilinda hisia zako na mawazo kutoka kwenye uoga kuhusu masumbuko ya haya maisha"