sw_tn/phm/front/intro.md

2.4 KiB

Utangulizi wa Filemoni

Sehemu ya 1: Utangulizi wa jumla

Muhtasari wa kitabu cha Filemoni

  1. Paulo anamsalimia Filemoni (1:1-3)
  2. Paulo anamuuliza Filemoni kumhusu Onesimo (1:4-21)
  3. Hitimisho (1:22-25)

Nani aliandika kitabu cha Filemoni?

Paulo alikiandika kitabu cha Filemoni. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alitokea mji wa Tarso. Kabla ya kuwa Mkristo alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika himaya nzima ya Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu

Paulo alikuwa gerezani alipoandika barua hii.

Kitabu cha Filemoni kinahusu nini?

Paulo aliandika barua hii kwa mwanaume aliyeitwa Filemoni. Filemoni alikuwa Mkristo aliyeishi katika jiji la Kolosae. Alikuwa na mtumwa aliyeitwa Onesimo. Onesimo alikuwa amemtoroka Filemoni na kuna uwezekano alikuwa pia amemuibia kitu.Onesimo alienda Roma na kumtembelea Paulo gerezani.

Paulo alimuambia Filemoni kwamba alikuwa anamtuma Onesimo kurudi kwake. Filemoni alikuwa na haki ya kumuua Onesimo kulingana na sheria za Warumi lakini Paulo akamsihi Filemoni kumkubali kama ndugu Mkiristo na akamshauri kumruhusu Onesimo kurudi kumsaidia Paulo gerezani

Kichwa cha kitabu hiki kinastahii kutasiriwa namna gani?

Watafsiri wanaweza kukiita hiki kitabu kutumia jina lake la kitamaduni, "Filemoni", ama wanaweza kuchagua kichwa kinachoeleweka wazi kama "Barua ya Paulo kwa Filemoni" ama "Barua Paulo alimwandikia Filemoni." (Tazama: rc://*/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni.

Je, barua hii inahalalisha utumwa?

Paulo alimtuma Onesimo kurudi kwa bwana wake. Hii haimaanishi kwamba alihalalisha utumwa. Paulo alizungumzia kuhusu watu kumtumkia Mungu katika hali zozote wangejipata ndani.

Paulo anamaanisha nini kwa maneno "ndani ya Kristo" na "Ndani ya Bwana"?

Paulo alitaka kuelezea wazo la kuwa na ushirika wa karibu sana kati ya muumini na Kristo. Tafadhali tazama utangulizi wa kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi kuhusu kauli hii.

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Umoja na wingi wa "wewe" na "nyinyi"

Katika kitabu hiki, neno "mimi" linaashiria Paulo. Neno "wewe" linaashiria Filemoni isipokuwa katika sehemu mbili 1:22 na 1:25. Hapa "nyinyi" huashiria Filemoni na waumini waliokutana katika nyumba yake.Tazama: [[rc:///ta/man/translate/figs-exclusive]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-you]])