sw_tn/num/03/44.md

2.0 KiB

BWANA

Neno "BWANA" ni jina la Mungu ambalo alilitumia wakati alipojifunua kwa Musa kwenye kile kichaka kilichowaka moto. Jina "BWANA" linatokana na neno ambalo linamaanisha, "kuwa" au "kuwepo." Linaweza kumaanisha "Yeye ndiye" au "Mimi ndiye" au "Yeye anayewezesha vitu kuwepo". Jina hili linafunua ukweli wa Mungu kuwa alikuwepo na ataendelea kuwepo daima. Jina hili linaandikwa kwa herufi kubwa kubwa ili kulitofautisha na neno Bwana ili kuonyesha heshima.

Musa

Musa alikuwa nabiina kiongozi wa Waisraeli kwa zaidi yamiaka 40. WakatiMusa alipokuwa mtoto mchanga: wazazi wake walimweka kwenye kikapu kisha kumtupa kwenye majani ya Mto Naili ili kumficha ili Farao Mmisiri asimwone. Umbu lake Miriamu alimtazama pale. Maishsa ya Musa yalisalimika pale binti wa Farao alipomwona na umchukua kisha akampeleka ikulu kulelewa. Mungu alimchagua Musa kuwaokoa wana wa Israeli kutoka utumwani na kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi. Baada ya Waisraeli kutoka Misri; wakati wakizungukazunguka jangwani,Mungu alimpatia Musa vidonge viwili vya mawe vilivyokuwa vimeandikwa amri kumi za Mungu. Karibu na mwisho wa maisha yake, Musa aliona ile nchi ya ahadi, lakini Mungu hakumruhusu kuingia pale kwa sababu alishindwa kutii.

Mlawi, Lawi

Lawi alikuwa mmoja wa wana kumi n a mbili wa Yakobo au Israeli. Neno "Mlawi" linamaanisha mtu ambaye anatoka kwenye ukoo wa Lawi. Walawi waliajibika kulitunza hekalu na kuendesha ibaada za kidini, ambazo zilijumuisha sadaka na dhabihu na maombi. Makuhani wote wa Kiyahudi walikuwa Walawi, waliokuwa wametokana na Lawi. Lakini si Walawi wote walikuwa makuhani. Makuhani wa Kilawi walikuwa wametengwa na kuwekwa wakfu kwa ajili ya kazi maalumu ya kumtumikia Mungu hekaluni. Kuna watu wawili pia waliojulikana kwa jina la "Lawi" wanaonekana kwenye ukoo wa Yesu katika injili ya Luka. Mwanafunzi wa Yesu aitwaye Mathayo pia aliitwa Lawi.

Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli

Jina "Israeli" ni jina ambalo Mungu alimpatia Yakobo. Linamaanisha, "aliyemng'ang'ania Mungu. Wana wa uzao wa Yakobo walijulikna kama "Watu wa Israeli," "taifa la Israeli," au "Waisraeli"