sw_tn/neh/01/01.md

1.2 KiB

Nehemia .....Hakalia .... Hanani

Haya ni majina ya watu

katika mwezi wa Kisleu

'Kislev' ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiebrania. Ni wakati wa mwisho wa Novemba na sehemu ya kwanza ya Desemba kwenye kalenda za Magharibi.

katika mwaka wa ishirini

Nehemia akimaanisha idadi ya miaka ambayo Artaxerxes alikuwa ametawala akiwa mfalme. AT 'mwaka wa ishirini wa utawala wa Artaxerxes, Mfalme wa Uajemi

mji mkuu wa Sushani

Hii ilikuwa moja ya miji ya kifalme ya wafalme wa Kiajemi, iliyo katika nchi ya Elamu. Ilikuwa jiji kubwa, yenye ngome yenye kuta za juu zilizozunguka.

mmoja wa ndugu zangu

Hanani alikuwa ndugu wa Nehemia wa kiroho.

Hanani, alikuja pamoja na watu wengine kutoka Yuda

Hanani alikuja kutoka Yuda na watu wengine'

Wayahudi waliopona, Wayahudi waliosalia waliokuwa huko

Maneno haya mawili yanataja kundi moja la watu. Maana inawezakuwa ni 1) Wayahudi wachache ambao walichukuliwa kama wahamisho Babeli lakini waliokoka na kurudi kuishi Yerusalemu au 2) Wayahudi wachache ambao waliokoka kutoka kwa wale waliokuwa wakijaribu kuwapeleka uhamishoni huko Babiloni na hivyo wakaa Yerusalemu. Kwa kuwa haijulikani wapi walipokimbia, inaweza kuwa bora si kutaja katika tafsiri. AT "Wayahudi ambao waliokoka uhamisho na waliobaki Yerusalemu'