sw_tn/mrk/09/intro.md

1.8 KiB

Marko 09 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"kugeuka sura"

Maandiko mara nyingi huzungumzia utukufu wa Mungu kama mwanga mkubwa, wenye nguvu. Watu wanapoona mwanga huu, wanaogopa. Marko anasema katika sura hii kwamba mavazi ya Yesu yalikuwa na mwanga huu wa utukufu kiasi cha kuwawezesha wafuasi wake kuona kwamba Yesu kweli alikuwa Mwana wa Mungu. Wakati huo huo, Mungu aliwaambia kwamba Yesu alikuwa Mwana wake. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/glory]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/fear]])

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Neno la kukaza ukweli la kupita ukweli

Yesu alisema mambo ambayo hakutarajia wafuasi wake kuelewa kwa kweli. Wakati aliposema, "Ikiwa mkono wako unakukosesha, uukate" (Marko 9:43), alikuwa akizidisha sana ili waweze kujua kwamba wanapaswa kuacha mbali na chochote kilichowaanya kutenda dhambi, hata kama ni kitu walipenda au walidhani walihitaji.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Eliya na Musa

Eliya na Musa ghafla wanaonekana kwa Yesu, Yakobo, Yohana, na Petro, na kisha kutoweka. Wote wanne waliona Eliya na Musa, na kwa sababu Eliya na Musa walizungumza na Yesu, msomaji anapaswa kuelewa kwamba Eliya na Musa walionekana kimwili.

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe "Mwana wa Binadamu" katika sura hii (Marko 9:31). Lugha yako huenda haiwezi kuwaruhusu watu kujizungumzia wenyewe kana kwamba wanaongea juu ya mtu mwingine. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/sonofman]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-123person]])

Kitendawili

Kitendawili ni taarifa ya kweli inayoonekana kuelezea kitu kisichowezekana. Yesu anatumia kitendawili wakati anasema, "Ikiwa mtu anataka kuwa wa kwanza, lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote" (Marko 9:35).

<< | >>