sw_tn/mrk/01/intro.md

969 B

Marko 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi kwa upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hii kwa mashairi katika 1:2-3, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

"Unaweza kunifanya kuwa safi"

Ukoma ulikuwa ugonjwa wa ngozi ambao ulimfanya mtu asiwe msafi na asiweze kumwabudu Mungu vizuri. Yesu anaweza kufanya watu kuwa "safi" au wenye afya kimwili au pia kuwa "safi" au wenye haki na Mungu kiroho . (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/clean)

"Ufalme wa Mungu umekaribia"

Wasomi wanajadiliana ikiwa "Ufalme wa Mungu" ulikuwapo wakati huu au bado unakuja. Tafsiri za Kiingereza mara nyingi hutumia maneno "karibu," lakini hii inaweza kusababisha ugumu kwa watafsiri. Matoleo mengine hutumia "unakuja" na "umekaribia."

| >>