sw_tn/mic/04/09.md

1.0 KiB

Sasa, kwa nini unapiga kelele kwa sauti kuu?

Mika anawatania watu, kujaribu kuwafanya kufikiria kuhusu kwa nini Mungu anashughulika nao katika njia hii. "Sasa, unapiga kelele kwa sauti kuu."

Je! Hakuna mfalme miongoni mwenu? Je! Mshauri wako amekufa? Je! Hii ndiyo sababu uchungu umekushika kama yule mwanamke katika kuzaa?

Mika anaendelea kuwahutubia watu katika sauti ya mzaha. Jibu la haya maswali ni hapana. Mfalme na washauri bado wapo huko, lakini wako kama hawana maana na wasio na matumaini. "Hivyo kwa nini unaomboleza sasa? Je! Ni kwa sababu hauna mfalme? Je! watu wako wenye hekima wamekufa? Unalia kwa sauti kuu kama mwanamke anayezaa mtoto."

Kuwa katika uchungu na kuzaa, binti wa Sayuni, kama mwanamke mwenye uchungu

Mika anatumia picha ya mwanamke katika kuzaa kusisitiza masumbuko makali ya uhamishoni. Anamaanisha kwamba watakuwa katika uchungu kwa sababu Mungu anawaadhibu kwa kuwapeleka mbali na Israeli. Wengi wao hawatakuja nyumbani tena.

Huko utaokoka. Huko Yahwe atakuokoa

"Huko Yahwe atakuokoa"