sw_tn/mic/04/01.md

612 B

mlima wa nyumba ya Yahwe utakuwa imara

"Yahwe atauimarisha mlima ambapo hekalu lake lilipojengwa"

juu ya milima mingine

Hii inamaanisha Mlima Sayuni utakuwa wa muhimu zaidi ya milima yote. Pia inaweza kumaanisha kwamba huu mlima utakuwa mrefu zaidi katika dunia, sio katika eneno pekee.

utakuwa imara juu ya milima mingine

"utaheshimiwa zaidi kuliko mlima mwingine wowote"

watu watatiririka kuuendea

Watu wa mataifa wataenda kwenye mlima wa Yahwe kama mkondo utiririkiao. Hii inamaanisha kwamba watu wengi wataenda. "watu wa mataifa watatiririka kama mto kuuendea" au "watu wa mataifa watauendea"