sw_tn/mat/11/28.md

36 lines
1.3 KiB
Markdown

# Sentensi unganishi
Yesu anamalizia kuongea na makutano.
# ninyi nyote
Viwakilishi vyote vya "niniyi" ni vya wingi
# mnaolemewa na mzigo mizito
Yesu anaongea kwa watu kama na wanyama, amabao bwana zao wamewabebesha mizigo migongoni mwao. Hii ni sitiari kwa ajili ya Sheria na kanuni ambaazo viongozi wa Kiyahudi waliwabebesha watu ili kuzitii. "msumbukao na sheria ambazo mmebeshwa na viongozi wa dini"
# Nitawapumzisha
''Nitawaruhusu nyinyi kupumzika kazi na mizigo''
# Mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo
Hapa neno"mpole" na "mnyenyekevu wa moyo" ki msingi yanamaanisha kitu kilekile. Yesu anayaunganisha kuongeza msisitizo kuwa atawajali kwa upole zaidi kuliko vioingozi wa . dini. "mimi ni mpole na mnyenyekevu" au "mimi ni mpole sana"
# Jitieni nira yangu
Yesu anaendelea kutumia sitiari. Yesu anawakaribisha watu kuwa wanafunziwake na kumfuata"
# mtapata pumziko la nafsi zenu
Hapa "nafsi" inamaanisha mtu kamili. "mtapumzikia ninyi wenyewe" au "mtaweza kupumzika"
# kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi
Virai vyote hivi vinamaanisha kitu kilekile. Yesu anasisitiza kuwa ni rahisi kumtii yeye kuliko sheria za Wayahudi. "kile nitakacho wabebesha kitakuwa ni chepesi"
# Mzigo wangu ni mwepesi
Neno "mwepesi" hapa ni kinyume cha kizito, siyo kinyume cha giza.