sw_tn/mat/09/20.md

44 lines
1.3 KiB
Markdown

# Sentensi unganishi
Hii inafafanua jinsi Yesu alivyomponya mwanamke mwingine wakati akiwa njiani kwenda kwa afisa wa Kiyahudi
# Tazama
Neno "tazama" linadokeza juu ya mtu mwingine katika hadithi. Lugha yenu inaweza kuwa na njia nyingine ya kufanya hivi
# alikuwa anatokwa damu
"kutokwa damu mfululizo"Yawezekana alikuwa akitokwa damu kwenye tumbo lake ingawa haikuwa kipindi cha kawaida yake. Baadhi ya tamaduni yawezekana wana namna nzuri ya kueleza tatizo hili.
# miaka kumi na mbili
"miaka 12"
# vazi
"kanzu"
# Endapo nitagusa vazi lake, nami nitapata uponyaji
Alifikiria hivi kabla hajamgusa Yesu. Unaweza kuiweka sentensi hii mwanzoni.
# Endapo nitagusa vazi lake
Kwa mjibu wa sheria za Kiyahudi, kwa sababu ya kutokwa na damu hakutakiwa kumgusa yeyote mtu yeyote. Anagusa vazi la Yesu ili nguvu za Yesu zimponye alidhani kuwa Yesu hatagundua kuwa ameguswa
# Lakini
"Badala" Kile mwanamke alichotumaini kutokea hakikutokea.
# Binti
Mwanamke hakuwa mtoto halisi wa Yesu. Yesu alikuwa akiongea naye kwa upole. Ikiwa hii inachanganya, inaweza kutafsiriwa "kijana wa kike" au hata kutolewa.
# imani yako imekufanya upone
"Kwa sababu uliniamini, Nitakuponya"
# Muda huo huo mwanamke alipokea uponyaji
Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo tendaji. "Yesu alimponya hapohapo"