sw_tn/mat/05/01.md

32 lines
1.0 KiB
Markdown

# Sentensi unganishi
Huu ni mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi ambayo Yesu alianza kuwafundisha wanafunzi wake. Sehemu hii huendelea hadi mwisho wa sura ya 7 na mara kwa mara huitwa mahubiri ya Mlimani.
# Maelezo ya jumla
Katika msyari wa 3, Yesu anaanza kueleza tabia za watu ambao wamebarikiwa.
# Akafunua kinywa chake
"Yesu alianza kunena."
# aliwafundisha
Neno "aliwa" humaanisha wanafunzi wake.
# maskini katika roho
Hii inamaanisha mtu ambaye ni mnyenyekevu. "wale ambao wanajua wanamhitaji Mungu."
# Kwa kuwa uflmeme wa mbinguni ni wao
Hapa "ufalme wa mbinguni" humaanisha utawala wa Mungu kama mfalme. Kirai hiki kiko katika kitabu cha Mathayo tu. Kama inawezekana weka "mbinguni" katika tafsiri yako. "kwa kuwa Mungu wa mbinguni atakuwa mfalme wao."
# wale ambao wana huzunika
Sababu zinazopelekea kuwa wenye huzuni ni 1) hali ya dhambi ya ulimwengu au 2) dhambi zao au 3) kifo cha mtu. Usieleze bayana sababu ya kuhuzunika isipkuwa lugha yako inataka hivyo.
# watafarijiwa
Hii inaweza kuelezwa katika namna ya mfumo tendaji. "Mungu atawafariji."