sw_tn/mat/03/01.md

28 lines
1.3 KiB
Markdown

# Taarifa kwa ujumla:
Huu ni mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi mahali ambapo mwandishi anaisimulia huduma ya Yohana Mbatizaji. Katika mst. 3. mwandishi anamnukuu nabii Isaya kuonesha kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa mjumbe aliyechaguliwa na Mungu kuandaa huduma ya Yesu.
# Katika siku hizo
Hii ni miaka mingi baada ya Yusufuna familia kuondoka Misri na kwenda Nazareti.Hii pengine karibu na wakati ambao Yesu alianza huduma yake. "Baadaye" au "Miaka kadhaa baadaye."
# Tubuni
Hii iko katika wingi. Yohana anazungumza na umati.
# ufalme wa mbinguni umekaribia
Kirai "ufalme wa mbinguni" humaanisha Mungu kutawala kama mfalme. Kirai hiki kiko katika kitabu cha Mathayo tu. Kama inawezekana, tumia neno "mbinguni" katika tafsiri yako. "Mungu wetu uliye mbinguni baada ya muda mfupi atajionesha mwenyewe kuwa mfalme."
# Kwa kuwa huyu ndiye aliyenenwa na nabii Isaya akisema
Hii inaweza kuelezwa katika nmna iliyo tendaji. "Kwa kuwa Isaya nabii alikuwa anamnena Yohana Mbatizaji wakati aliposema."
# Sauti ya mtu
Hapa "sauti" humaanisha nafsi yote. "Kuna mtu."
# Tengenezeni njia ya Bwana, nyosheni njia yake
"Andaeni njia ya Bwana, nyosheni njia yake." Hii ni sitiari ya ujumbe wa Yohana ambao unawita watu kujiandaa na ujio wa Yesu kwa kufanya toba ya dhambi zao. "Badilika katika maisha yako hivyo utakuwa tayari wakati Bwana ajapo."