sw_tn/luk/22/07.md

1.2 KiB

Maelezo ya ujumla:

Hii ni sehemu nyingine ya simulizi. Yesu anawatuma Petro na Yohana kuandaa kwa ajili ya chakula cha Pasaka. Mstari wa saba utatupa habari au taarifa za msingi kuhusu simulizi inavyoanza.

Siku ya mkate usiyotiwa chachu

"Siku ya mkate bila hamila" au "Siku ya chapati." Hii ilikuwa ni siku ambayo Wayahudi wangetoa nje ya nyumba zao mikate yote ambayo ilikuwa imetengenezwa na hamila. Kisha wangesherehekea sikukuu ya mkate usiyotiwa chachu au hamila kwa siku saba.

kondoo wa Pasaka lazima atolewe

Kila familia au kikundi cha watu wangemchinja kondoo na kumla pamoja, hivyo kondoo wengi sana walichinjwa. Tafsiri mbadala: "watu ilikuwa lazima wachinje kondoo kwa ajili ya chakula cha Pasaka."

ili tuje tukile

Yesu alikuwa anawajumuisha Petro na Yohana aliposema "tu.." Petro na Yohana wangekuwa sehemu ya kundi ambalo lingekula chakula kile.

mkatuandalie

Hili ni neno la kiujumla linalomaanisha "fanya tayari." Yesu si kwamba alikuwa akiwaambia Petro na Yohana kufanya mapishi yote.

unataka tufanyie hayo maandalizi

Neno "tu.." halimuhusishi Yesu. Yesu asingekuwa sehemu ya kundi ambalo lingeandaa chakula kile.

tufanye maandalizi

"kufanya maandalizi ya chakula" au "kuandaa chakula"