sw_tn/luk/12/13.md

1011 B

Habari za Jumla

Hii ni katizo kwa mafundisho ya Yesu. Mtu mmoja alimuomba Yesu amfanyie kitu na Yesu akamjibu.

Mtu

Maana inayowezekani ni 1) Hii ni namna ya kuongea na mtu mgeni au 2) Yesu anamkemea yule mtu. Labda lugha yenu ina njia mbadala ya kuongea na watu kwa namna ya njia hizi mbili. Watu wengine hawatafsiri neno hili kabisa.

Ni nani aliyeniweka kuwa mwamuzi au mpatanishi kati yenu?

Yesu alitumia swali kumfundisha huyo mtu. " Mimi siyo mwamuzi wenu au mpatanishi" . Lugha zingine hutumia wingi wa maneno ya "Yenu" au "Wenu"

Ndipo akawaambia

Neno "akawaambia" hapa huenda inarejea umati wote wa watu.

jihadharini na kila namna ya tamaa

"Jichungei na kila aina ya uchoyo". "Msijiruhusu kupenda kuwa vitu"au " Msiruhusu tamaa ya kuwa na vitu vingi iwatawale"

uzima wa mtu

Hii ni kauli ya jumla za ukweli. Haimrejei mtu yeyote maalum. Lugha nyingine zina jinsi ya kuelezea .

wingi wa vitu alivyo navyo

"Ni kiasi gani vya vitu anavyomiliki" au "kiasi gani ya mali anayomiliki"