sw_tn/luk/03/08.md

867 B

Zaeni matunda yanayoendana na toba

Katika mfano huu, tabia ya mtu inalinganishwa na mti. Kama tu kwa mmea linavyotarajiwa kuzaa tunda linaloendana na aina ya mmea, mtu ambaye anasema kwamba ametubu, anatarajiwa kuishi kwa haki. AT: "Zaeni aina ya tunda linaloonyesha kwamba umetubu" au "fanya mambo mema yanayoonyesha kwamba umegeuka kutoka katika dhambi zako."

Mkisema wenyewe ndani yenu

"Kusema mwenyewe" au "kufikiri mwenyewe"

Tuna Ibrahimu aliye baba yetu

"Abrahamu ni Baba yetu" au Sisi ni uzao wa Ibrahimu. "kama inaeleweka kwanini wangesema hili, unaweza pia kuongeza habari imaanishayo: "Hivyo Mungu hatatuadhibu sisi."

Kumwinulia Ibrahimu watoto

Nahau hii inamaanisha "Umba watoto kwa ajili ya Ibrahimu" au "sababisha watu kuwa wafuasi wa Ibrahimu."

Kutokana na mawe haya

Labda Yohana alikuwa anamaanisha mawe halisi kando ya Mto Yordani.