sw_tn/luk/01/18.md

1.0 KiB

Namna gani naweza kujua hili?

"Jinsi gani naweza kujua kwa hakika kwamba ulichosema kitatokea"? "kujua" kunamaanisha kujifunza kupitia uzoefu, akipendekeza Zakaria alikuwa akiuliza kutokana ishara kama uthibitisho. Hii inaweza kusemwa wazi kama: NI: "unaweza kufanya nini kuthibitisha kwangu kwamba hiki kitatokea?"

Mimi ni Gabrieli, ambaye nasimama katika uwepo wa Mungu

Hii inasemwa kama kukemewa kwa Zakaria. Uwepo wa Gabrieli, unakuja moja kwa moja kutoka kwa Mungu, itakuwa inatosha kumthibitishia Zakaria.

ambaye husimama

"ambaye hutumika"

nilitumwa kuzungumza na wewe

Hii inaweza. kusemwa kwenye mtindo wa kutenda. NI: "Mungu alinituma kusema kwako."

tazama

Neno "tazama" hapa linatutaarifu kuwa makini kwa taarifa zinazofuata za ku.shangaza

ukimya, kutoweza kuzungumza

Hii inamaanisha kitu kilekile, na vilirudiwa kusisitiza ukamilifu wa ukimya wake. NI: "kutoweza kuzungumza kabisa" au "hawezi kuzungumza kwa vyovyote."

kutoamini maneno yangu

"usiamini yale niliyosema"

kwa wakati sahihi

"kwa wakati ulioandaliwa"