sw_tn/luk/01/01.md

1.3 KiB

Taarifa kwa Ujumla

Luka anaeleza kwanini anamwandikia Theofilo.

mada

"taarifa" au "simulizi za kweli"

kati yetu

Neno "yetu" katika kauli hii linaweza au haliwezi kutomhusisha Theofilo.

Alikabidhi kwetu sisi

"Sisi" katika kauli hii Theofilo hahusiki.

Kabidhiwa kwao

"kupewa wao" au "iliyotolewa kwao"

Watumishi wa ujumbe

Unaweza kuhitaji kupambanua kwamba ujumbe ni nini. NI: "kumtumikia Mungu kwa kuwaambia watu habari zake" au "kufundisha watu habari njema kuhusu Yesu"

Ilichunguzwa kwa uangalifu

"kutafiti kwa makini." Luka alikuwa makini kutafuta uhakika wa kile kilichotokea. Huenda alizungumza na watu mbalimbali ambao waliona kilichotokea kuhakikisha anachokindika kuhusu tukio hili ni sahihi.

Mheshimiwa sana Theofilo

Luka alisema hivi kuonesha heshima na taadhima kwa Theofilo. Hii inaweza kumaanisha kwamba Theofilo alikuwa afisa mhimu serikalini. Sehemu hii tumia mfumo unaotumika kwenye utamaduni wako kumwongelea mtu mwenye mamlaka ya juu. Baadhi ya watu wanaweza kupendelea pia kuweka salamu mwanzoni na kusema "kwa ... Theofilo" au "Mpendwa ... Theofilo."

Mheshimiwa sana

"mheshimiwa" au "muungwana"

Theofilo

Jina hili linamaana "rafiki wa Mungu." Linaweza likaweka wazi tabia ya mtu huyu au inaweza kuwa ndilo jina lake halisi. Tafsiri nyingi limetumika kama jina lake.