sw_tn/jud/01/12.md

1.3 KiB

sentensi unganishi

Yuda anatumia mifano mingi kumfafanua mtu asiye na utaua. Anawambia waamini jinsi wanvyo paswa kumtambua mtu huyu miongoni mwao.

Hawa ni wale

"Hawa" ina rejea kwa watu waovu.

miti iliyopukutika isiyo na matunda

Kama baadhi ya miti isiyozalisha matunda katika mwisho wa majira ya joto, hivyo watu hawa waovu hawana imani na kazi za haki.

bila matunda, kufa mara mbili

Kama miti ambayo imeuawa mara mbili kama vile kwa baridi usingeweza kutoa matunda, kwa hiyo watu waovu hawana thamani na hawana maisha ndani yao.

iliyong'olewa na mizizi

Kama miti ambayo imeng'olewa kwenye udongo na mizizi yake, watu waovu wametenganishwa kutoka kwa Mungu ambaye ni chanzo cha maisha.

pori la mawimbi ya bahari

Kama mawimbi ya bahari yanayosukumwa na upepo mkali, hivyo watu waovu hawakuwa na msingi wa imani na walihamishwa kwa urahisi katika mwelekeo mwingi.

yakitoa aibu yao wenyewe

Kama upepo usababishao pori la wimbi kukoroga povu chafu, hivyo watu hawa kwa kupitia mafundisho ya uongo na matendo huwa aibisha wenyewe. AT: "kama vile wimbi huleta povu na uchafu, watu hawa wanachafua wengine kwa aibu yao."

Nyota zinazo randaranda, ambao weusi wa giza umetunzwa kwa ajili yao milele

Kama vile nyota zitembeavyo angani na kufanya ugumu kuzifuata, hivyo na wewe usiwafuate watu hao.