sw_tn/jos/14/02.md

1.1 KiB

Urithi wao ulichaguliwa kwa kupiga kura

Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. Eliazeri, Yoshua na viongozi wa makabila walipiga kura kuamua urithi wao."

kwa mkono wa Musa

Hapa neno "mkono" unamwakilisha Musa mwenyewe na ina maana ya Yahweh alimtumia Musas kama wakala ili kutoa agizo hili.

Musa alikuwa amewapa urithi makabila mawili na nusu ng'ambo ya Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi wowote

Makabila mawili na Nusu yalipewa urithi ng'ambo ya Yordani, lakini kwa Walawi hawakupewa urithi wowote. Nchi ambayo Musa aliyapa makabila inasemwa kana kwamba ni urithi ambao walipokea kama miliki yao ya kudumu.

Na hakuna sehemu yoyote ya urithi waliyopewa Walawi katika nchi

Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Na Musa hakuwapa sehemu yoyote ya urithi kwa Walawi katika nchi."

sehemu ya nchi

Kipande cha ardhi

lakini walipewa miji ya kuishi ndani yake

Kitenzi huenda kimetolewa kwa maelezo yaliyotangullia."lakini aliwapa miji fulani ili kuishi ndani yake."

maeneo ya malisho

haya ni mashamba ya nyasi kwa ajili kulishia mifugo.

riziki zao

hivi ni vitu walivyohitaji ili waweze kuhudumia familia zao.