sw_tn/jos/07/14.md

32 lines
1.2 KiB
Markdown

# Sentensi kiunganishi
Yahweh anaendelea kumwambia Yoshua kile anachopaswa kuwaambia watu.
# mtajisogeza wenyewe kwa makabila
Kulikuwa na makabila kumi na mawili yaliyowafanya watu wa Israeli. Kifungu cha maneno "kwa makabila" kina maana ya "kila kabila"
# Kabila lile ambalo Yahweh atalichagua litasogea karibu kwa koo zake
Kabila hujengwa na makabila mengi. "Kutoka katika kabila ambalo Yahweh amelichagua, kila kabila litakaribia,"
# Kabila ambalo Yahweh atalichagua
Viongozi wa Israeli watapiga kura, na kwa kufanya hivi, wangejifunza ni kabila gani Yahweh alikuwa amelichagua.
# Ukoo ule ambao Yahweh atauchagua lazima usogee karibu kwa nyumba
Ukoo ulijengwa na familia/nyumba kadhaa. "Kutoka katika ukoo ambao Yahweh ameuchagua, kila nyumba itasogea karibu."
# Nyumba ambayo Yahweh ataichagua lazima isogee karibu kwa mtu mmoja mmoja
Nyumba iliundwa na watu kadhaa. "Kutoka katika nyumba ambayo Yahweh ameichagua, kila mtu atasogea karibu"
# Itakuwa hivi mtu yule atakayechaguliwa
Maneno haya yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji "Yeye ambaye Yahweh anamchagua"
# amelivunja agano la Yahweh
Kuvunja agana kuna maana ya kutolitii. "Ameliasia agano la Yahweh"