sw_tn/jos/07/10.md

28 lines
1.0 KiB
Markdown

# Maelezo ya jumla
Yahweh anamwambia Yoshua kwanini Israeli imelaaniwa.
# kwanini umelala kifudifudi?
Mungu alitumia swali hili kumkemea Yoshua kwa kulala kifudifudi. "Acha kulala hapo kifudifudi katika uchafu!."
# vitu vilivyokuwa vimetengwa
Hivi ni vitu "viliwekwa kwa ajili ya kuharibiwa" kutoka katika 6:17 "Vitu vilivyolaaniwa" au "Vitu vile ambavyo Mungu amevilaani"
# Wameiba na kisha pia wakaficha dhambi yao
Kuficha dhambi ina maana ya kujaribu kuwafanya watu wengine wasijue kuwa wametenda dhambi. "Wameviiba vitu vile na kisha walijaribu kuwaficha watu wasijue kuwa wametenda dhambi"
# hawataweza kusimama mbele za maadui zao
Kusimama mbele ya maadui zao kuna maana ya kupigana kwa mafanikio dhidi ya maadui zao. Hivyo ina maana ya "hawataweza kupigana kwa mafanikio dhidi ya maadui zao" au "hawataweza kuwashinda maadui zao."
# Walitega migongo yao kwa maadui zao
Kutega migongo kuna maana ya kukimbia mbali kutoka kwa maadui zao.
# Sitakuwa pamoja nanyi tena
Kuwa pamoja na Israeli kuna maana ya kuwasaidia Waisraeli. "Sitawasaidieni tena."