sw_tn/job/03/04.md

32 lines
1.3 KiB
Markdown

# Habari za Jumla:
Semi zote katika mistari hii ni matamanio kwamba siku ya kuzaliwa kwake Ayubu isingekuwako tena. Hii inaweza husika na siku, japokuwa katika wakati uliopita, hata kuwepo kwa namna fulani. ... "Natamani kwamba siku nilipozaliwa ingelikuwa giza."
# Siku hiyo na iwe giza ... wala mwanga usiiangazie
Vifungu hivi viwili vinaelezea giza la siku ya kuzaliwa kwake Ayubu, hivyo kurudia majuto ya Ayubu ya kuwa alikuwa amezaliwa.
# Siku hiyo na iwe giza
Hili ni tamanio la kutokuwepo tena siku hiyo. "ikiwezekana siku hiyo itoweke."
# Ishikwe na giza na kivuli la mauti liwe lake
Hapa giza na kivuli cha mauti vinazungumziwa kana kwamba ni watu ambao wanaweza kudai chochote kuwa ni mali yao. Neno "hii" inahusiana na siku ya kuzaliwa kwa Ayubu.
# kivuli cha mauti
Hapa kivuli kinawakilisha mauti yenyewe. "kifo kama kivuli"
# Wingu na likae juu yake
Hapa wingu linazungumziwa kana kwamba ni mtu ambaye anaweza kuishi juu ya siku ya kuzaliwa kwake Ayubu. "Ikiwezekana wingu liifunike hivyo hakuna mtu anayeweza kuiona"
# kila kitu kiifanyacho siku kuwa giza
Hii inamaanisha vitu vizuiavyo nje mwanga wa jua na kutengeneza giza. Hapa "nyeusi" inawakilisha giza.
# kiitishe
"itishe siku hiyo." Siku inazungumziwa kana kwamba ni mtu ambaye anaweza kutishwa na giza.