sw_tn/jhn/12/intro.md

2.6 KiB

Yohana 12 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka nukuu za Agano la Kale. Tafsiri ya ULB na nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari ya 12:38 na 40, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Mstari wa 16 ni ufafanuzi juu ya matukio haya. Inawezekana kuweka mstari huu mzima kwa mabano ili kuonyesha tofauti na maelezo ya habari.

Dhana maalum katika sura hii

Upako

Ilikuwa ni desturi kupaka mafuta mwili katika maandalizi ya kuizika. Hii kwa kawaida haingefanyika mpaka baada ya kifo cha mtu. Hii haikuwa nia ya Maria. Yesu anatumia matendo ya Maria kutabiri kuhusu kifo chake kilichokuwa kinakaribia. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/anoint]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/prophet]] and rc://*/ta/man/translate/figs-explicit)

Punda

Jinsi ambavyo Yesu aliingia Yerusalemu, akiwa amepanda mnyama, ilikuwa sawa na vile ambavyo mfalme angeingia katika mji baada ya ushindi mkubwa. Na kwa wafalme wa Israeli, ilikuwa desturi kupanda punda badala ya farasi. Mathayo, Marko, Luka, na Yohana wote waliandika juu ya tukio hili, lakini hawakupa maelezo sawa. Mathayo aliandika kuhusu kuwepo kwa punda na mwana-punda, lakini haijulikani ni yupi ambaye Yesu alipanda. Ni bora kutafsiri kila moja ya vifungu hivi kama inavyoonekana katika ULB bila kujaribu kuwafanya wote kusema jambo sawa. (Angalia: Mathayo 21: 1-7 na Marko 11: 1-7)

Mwangaza

Mwangaza ni mfano ya kawaida katika Maandiko yaliyotumiwa kuonyesha haki. Mwangaza pia hutumiwa kuonyesha njia ya haki na kuonyesha maisha ya haki. Giza hutumiwa mara nyingi kama mfano ya kuonyesha dhambi au uovu. (See: [[rc:///tw/dict/bible/other/light]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/righteous]], [[rc:///tw/dict/bible/other/darkness]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]] and rc://*/tw/dict/bible/kt/unrighteous)

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

"Ili atukuzwe"

Unabii wa Yesu kuhusu kutukuzwa kwake ni maelezo juu ya kifo chake. Wanafunzi hawakuelewa kwamba kifo chake kingemtukuza, lakini kilifanyika vivyo hivyo. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/glory]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-irony]])

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kitendawili

Kitendawili ni taarifa inayoonekana kuwa ya ajabu, ambayo ni kana kwamba inajikana yenyewe, lakini kwa hakika sio ya ajabu. Kitendawili kinatokea katika 12:25: "Yeye anayependa maisha yake ataipoteza, lakini anayechukia maisha yake katika ulimwengu huu ataichunga kwa uzima wa milele." Lakini katika 12:26 Yesu anaelezea maana ya kuchunga maisha ya mtu kwa ajili ya uzima wa milele. (Yohana 12: 25-26).

<< | >>