sw_tn/jhn/04/34.md

1017 B

chakula changu ni kufanya mapenzi yake aliyenituma na kutimiza kazi yake

"Chakula" hapa ni lugha ya picha inayowakilisha "kutii mapenzi ya Mugu." Kama vile ambavyo chakula kinavyo mtoshelea mwenye njaa, kutii mapenzi ya Mungu ndich kinachonitosheleza."

Je hamsemi

'Je hii sio miongoni mwa misemo yenu maarufu"

tazameni mashamba, kwa sababu yako tayari kwa mavuno

maneno haya mashamba na mazao yaliyo tayari yana lugha ya picha. Mashamba yanawakilisha watu wa mataifa. Na neno wako tayari linamaanisha utayari wa watu wa mataifu wa kupokea ujumbe wa Yesu kama vile mashamba yalivyo tayari kwa kuvunwa. "tazameni hawa watu wa mataifa!wako tayari kupokea ujumbe wangu, kama vile mazao katika mashamba yalivyo tayari kwa ajili ya kuvunwa."

Yeye avunaye anapokea posho na hukusanya matunda kwa uzima wa milele

Yesu anaonyesha kuwa kuna tuzo kwa wale "wanaofanya kazi katika mashamba" na kuwashirikisha ujumbe wake wengine. Na yule atakaye pokea ujumbe atapokea pia uzima wa milele ambao Mungu anawapa watu.