sw_tn/jer/16/19.md

1.3 KiB

Bwana, wewe ndiwe ngome yangu

Hapa Yeremia anaanza kuzungumza na Bwana.

ngome yangu, na kimbilio langu, na mahali pa usalama

Yeremia anazungumza juu ya Bwana kama mahali ambako adui hawezi kumshambulia. Anarudia wazo sawa mara tatu.

mwisho wa Dunia

"kila mahali duniani"

baba zetu walirithi udanganyifu

Hapa neno "udanganyifu" linamaanisha miungu ya uongo.

Ubatili mtupu; hakuna faida ndani yao

Hapa maneno "Wao" na "wao" yanataja miungu ya uongo ambayo mababu waliwafundisha kuamini. Maneno mawili yanamaanisha kuwa ni sawa, na pili kuelezea jinsi 'ni tupu.'

Watu hufanya miungu kwa ajili yao wenyewe?

Yeremia anauliza swali hili kusisitiza kwamba watu hawawezi kufanya miungu kwa ajili yao wenyewe. AT "Watu hawawezi kufanya miungu kwa ajili yao wenyewe."

Kwa hiyo tazama!

Hapa Bwana huanza kusema. Neno "tazama" linaongeza mkazo kwa ifuatavyo. AT "Kwa hiyo, kwa kweli,"

Nitawafanya wajue

Hapa neno "wao" linamaanisha watu kutoka mataifa. Bwana anarudia maneno haya kwa msisitizo.

mkono wangu na nguvu zangu

Hapa neno "mkono" linamaanisha nguvu na mamlaka. Maneno mawili yanamaanisha jambo sawa na kusisitiza nguvu kubwa za Bwana. AT "nguvu yangu kubwa."

watajua kwamba Yahweh ni jina langu

Hapa neno "jina" linahusu mtu mzima wa Yahweh. AT "watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wa kweli"