sw_tn/jdg/14/03.md

840 B

Je, hakuna mwanamke kati ya binti za ndugu zako, au kati ya watu wetu wote?

Waliuliza swali kwa kutoa maoni kuwa wanaweza kumtaftia Samsoni mke kati ya jamaa zao.

binti za ndugu zako

"binti" ni njia moja wapo ya kuelezea kuwa mwanamke huyu alikuwa hajaolewa.

Je! Utachukua mke kutoka kwa Wafilisti wasiotahiriwa?

Swali hili linaulizwa ili kumkemea Samsoni. "Hutakiwi kuoa mwanamke wa Kifilisti kwa sababu Wafilisti hawamwabudu Bwana"

Nichukulie kwa ajili yangu

Samsoni aliwaomba wazazi wake wazungumze na wazazi wa yule mwanamke kuhusu ndoa.

Ananipendeza mimi

Samsoni alifikiri kuwa binti yule ni mzuri. "Ananipendeza kwa namna alivyo mzuri"

suala hili

Hili ni ombi la Samsoni kuoa wanamke wa Kifilisti.

kwa maana alitaka kutengeneza mgogoro na Wafilisti

Kwa maana Bwana alitaka kutengeneza mgogoro na Wafilisti.