sw_tn/jdg/08/02.md

1.1 KiB

Taarifa ya jumla

Gideoni anawajibu watu wa Efraimu.

Nimefanya nini sasa kulinganisha na mlichofanya ninyi?

Gideoni anatumia swali kuonesha heshima kwa watu wa Efraimu. "Nimefanya mambo madogo gasa ukilinganisha na mliyofanya"

Je! Mavuno ya zabibu za Efraimu si bora zaidi kuliko mavuno ya zabibu ya Abiezeri?

"Mavuno ya Zabibu zenu watu wa Efraimu ni bora kuliko yetu sisi watu wa Abiezeri"

Je! Mavuno ya zabibu za Efraimu si bora zaidi kuliko mavuno ya zabibu ya Abiezeri?

Gideoni na jeshi lake kuwashinda Wamidiani kunafananishwa na mavuno ya zabibu. Watu wa Efraimi kumuua Orebu na Zeebu kunafananishwa na mavuno ya zabibu katika kipindi cha mavuno. "Jambo ambalo ninyi watu wa Efraimu mmefanya mwishoni mwa vita ni muhimu kuliko jambo ambalo sisi uzao wa Abiezeri tumefanya mwanzoni"

Abiezeri

Hili ni jina la mababu wa Gideoni. Gideoni alilitumia kuelezea uzao wa Abiezeri na nchi yao.

Orebu na Zeebu

Haya ni majina ya wanaume.

Mimi nimefanya nini ukilinganisha na ninyi?

Gideoni anatumia swali kuonesha heshima kwa watu wa Efraimu. "Nimefanya mambo madogo gasa ukilinganisha na mliyofanya"

Ikashuka chini

"ikapungua"