sw_tn/jdg/06/13.md

699 B

bwana wangu

Gidioni anatumia neno "bwana" kama njia ya unyenyekevu ya kumsalimia mgeni. Hakugundua kuwa anazungumza na Bwana kwa namna ya malaika.

Je, yako wapi matendo yake yote mazuri ambayo baba zetu walituambia, waliposema, 'Je! si Bwana aliyetukomboa kutoka Misri?'

Gidioni anatumia swali ili kuipinga sentensi ya mgeni kuwa Bwana yuko pamoja naye. Sentensi hii yaweza kuwa moja kwa moja kama "Hatujaona matendo makuu kama tuliyoambiwa na baba zetu kwamba Bwana aliwatoa Misri"

kututia mikononi mwa Midiani.

"kututia" inamaanisha Bwana aliruhusu Waisraeli washindwe.

kututia mikononi

"mkono" inawakilisha nguvu na utawala.

mwa Midiani

"Midiani" inawakilisha watu wa Midiani.