sw_tn/jas/front/intro.md

4.1 KiB

Utangulizi wa Yakobo

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Jumla

Muhtasari wa Kitabu cha Yakobo

  1. Salamu (1:1)

  2. Kujaribiwa na ukomavu (1:2-18)

  3. Kusikia na kulitenda neno la Mungu

  4. Imani ya kweli inaonekana kwa matendo

    • Neno la Mungu ( 1:19-27)
    • Sheria ya kifalme ya upendo (2:1-13)
    • Matendo (2:14-26).
  5. Matatizo katika jumuiya

    • Hatari za ulimi (3:1-12)
    • Hekima kutoka juu (3:13-18)
    • Tamaa za kidunia (4:1-12)
  6. Mtazamo wa Mungu kuhusu maamuzi yako

    • Majivuno juu ya kesho (4:13-17)
    • Onyo kuhusu utajiri(5:1-6)
    • Kuteseka na uvumilivu (5:7-11)
  7. Maonyo ya kumalizia

    • Viapo (5:12)
    • Sala na uponyaji (5:13-18)
    • Kujali kila mmoja (5:19-20)

Nani alikiandika kitabu cha Yakobo?

Mwandishi wa kitabu hiki anajitambulisha kama Yakobo. Kuna uwezekano Yakobo alikuwa ndugu wa kambo wa Yesu. Yakobo alikuwa kiongozi wa kanisa la mwanzo na mwanachama wa baraza la Yerusalemu. Mtume Paulo pia alimuita "mhimili" wa kanisa.

Huyu siye mtume Yakobo. Mtume Yakobo aliuwawa kabla ya barua hii haijaandikwa.

Kitabu cha Yakobo kinahusu nini?

Katika barua hii Yakobo anawapa moyo waumini waliokuwa wanateseka. Aliwaeleza kwamba Mungu hutumia mateso kuwafanya wawe Wakristo wakomavu. Yakobo pia anawaelezea umuhimu wa waumini kutenda mema. Aliandika mengi kuhusu jinsi waumini wanapaswa kuishi na kuwatendea wengine. Kwa mfano aliwaamuru watendeane haki, kutopigana na kutumia mali kwa hekima.

Yakobo aliwafunza wasomaji wake kutumia mifano mingi kutoka kwa mazingira. Kwa mfano katika 1:6, 11 na 3:1-12. Pia sehemu nyingi za barua hii zinafanana na yale Yesu aliandika kwenye Hotuba mlimani (Mathayo 5-7).

Akina nani walikuwa "Makabila kumi na mbili yaliyotawanyika?"

Yakobo alisema alikuwa anawaandikia "makabila kumi na mbili yaliyotawanyika"(1:1) Wasomi wengine wanafikiri kwamba Yakobo aliwaandikia Wakristo Wayahudi. Wasomi wengine wanafikiri kwamba Yakobo aliwaanndikia Wakristo wote kwa ujumla. Barua hii ni mojayapo ya "barua za jumla" kwa vile haikuandikiwa kanisa fulani ama mtu fulani.

Kichwa cha Kitabu hiki kitafsiriwe namuna gani?

Watafsiri wanaweza kukiita kitabu hiki kutumia kichwa chake cha asili "Yakobo" ama wanaweza kuchagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama "Barua kutoka kwa Yakobo" ama "Barua iliyoandikwa na Yakobo" (Tazama: rc://*/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamatudi

Je, Yakobo alitofautiana na Paulo kuhusu jinsi ya mtu kuhesabiwa haki mbele za Mungu?

Paulo alifundisha kwamba Wakristo wanahesabiwa haki kwa imani na siyo kwa vitendo. Inaonekana Yakobo anawafundisha Wakristo kwamba Wakristo wanahesabiwa haki kwa vitendo vyao. Hali hii inaweza kutatanisha. Lakini kuelewa kuzuri kuhusu kile Paulo na Yakobo walifundisha kunaonyesha kwamba hawakutofautiana. Wote walifundisha kwamba mtu anahitaji imani "ili ahesabiwa haki. Wote walifundisha pia kwamba imani ya kweli itamfanya mtu kutenda mema. Paulo na Yakobo waliyafundisha mambo haya kwa njia tofauti kwa sababu walikuwa na hadhira tofauti zilizotaka kujua vitu vingi kuhusu kuhesbiwa haki. (Tazama: [[rc:///tw/dict/bible/kt/justice]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/faith]] and rc://*/tw/dict/bible/kt/works)

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Watafsiri wanatakiwa kuashiria namna gani mipito kati ya mada za kitabu cha Yakobo?

Barua hii inabadilisha mada haraka. Wakati mwingine Yakobo hawaelezi wasomaji kwamba karibu anabadilisha mada. Inakubalika kuacha mistari kuonekana haina uhusiano. Ni busara kuweka kando aya kwa kuanzisha mistari mipya ama kuacha nafasi katikati ya mada.

Ni maswala gani muhimu katika maandishi ya kitabu cha Yakobo?

  • "Usitake kujua, mpumbavu, kwamba imani bila matendo ni bure."(2:20). Matoleo ya ULB, UDB na ya kisasa husoma hivyo. Lakini matoleo mengine ya zamani husoma, "Unataka kujua, Mpumbavu, kwamba imani bila matendo imekufa?" Kama kuna tafsiri ya Bibilia katika eneo kwa ujumla, watafsiri wanapaswa kuzingatia kutumia masomo yanayopatikana katika matoleo hayo.La sivyo, watafsiri wanashauriwa kufuata masomo ya kisasa.

(See: rc://*/ta/man/Translate/translate-textvariants)