sw_tn/isa/63/01.md

20 lines
845 B
Markdown

# Ni nani huyu ajaye kutoka Edomu ... Bosra
Isaya anazungumza kama mlinzi kwa kutumia mfumo wa swali na jibu kuwakilisha taarifa hii juu ya hukumu ya Yahwe kwa Edomu, adui wa Israeli. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Mimi, Yahwe, ninakuja kutoka Edomu, nikiwa nimevaa mavazi mekundu kutoka Bosra"
# Bosra
Huu ni mji mkuu wa Edomu.
# Ni Mimi
Hapa "Mimi" ina maana ya Yahwe.
# Kwa nini nguo zako ni nyekundu, na kwa nini ... kishinikizo cha zabibu
Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Wekundu katika nguo zako zinakufanya uonekane kana kwamba ulikuwa ukikanyaga ju ya zabibu katika kishinikizo cha zabibu"
# kishinikizo cha zabibu
Kishinikizo cha zabibu ni sehemu ya chini iliyochongwa kwa jiwe katika ardhi ambapo wafanyakazi hukanyaga zabibu kuziponda kwa miguu yao, ili kutoa juisi ya zabibu.