sw_tn/isa/51/23.md

20 lines
914 B
Markdown

# Maelezo ya Jumla
Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.
# Nitakiweka katika mkono wa msumbufu wako
Hii inazungumzia Yahwe kuwaadhibu adui zake kana kwamba alikuwa akienda kuwalazimisha kunywa kutoka katika kikombe kilichojaa hasira yake.
# Nitakiweka katika mkono wa msumbufu wako
Inadokezwa ya kwamba kwa kuweka kikombe cha hasira yake katika mkono wao Yahwe atakuwa anawalazimisha kunywa kile kilicho katika kikombe. "Nitawalazimisha wasumbufu wako kunywa kutoka katiika mvinyo wa bakuli la hasira yangu"
# msumbufu wako
Neno "wasumbufu" inaweza kuelezwa kwa kitenzi. "wale ambao wamekusumbua" au "wale ambao wamekusababisha kuteseka"
# ulifanya mgongo wako kama ardhi na kama mitaa kwa ajili yao kutembea juu
Hii inalinganisha namna adui zake walitembea juu ya migongo yao kwa namna watu wanavyotembea juu ya mitaa. "unalala katika mitaa ili maadui zako waweze kutembea juu ya migongo yako"