sw_tn/isa/51/21.md

28 lines
1.4 KiB
Markdown

# Maelezo ya Jumla
Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.
# wewe uliyekandamizwa na wewe uliyelewa
Yahwe anatumia neno "uliyekandamizwa" hapa kumaanisha watu wote waliokandamizwa. "nyie watu mliokandamizwa na walevi"
# wewe uliyelewa, lakini sio ulevi wa mvinyo
Hii inazungumzia watu kujifanya wamelewa kwa sababu wanateseka kana kwamba wamelewa kwa kulazimishwa kunywa bakuli ya hasira y Yahwe. "wewe ambaye umelewa kwa kunywa mvinyo wa bakuli la hasira ya Yahwe" au "wewe unayejifanya umelewa, kwa sababu umeteseka sana"
# Tazama, nimechukua kikombe cha kupepesuka kutoka mkononi mwako - bakuli, ambalo ni kikombe cha hasira yangu - ili kwamba
Hii inazungumzia Yahwe kutokuwa na hasira na watu wake kana kwamba hasira yake likuwa ujazo wa kikombe ambacho alikuwa akikichukua kutoka kwao. "Sitakuwa na hasira na wewe tena. Tazama, ni kana kwamba nimechukua kutoka kwako kikombe kilichokufanya upepesuke, yaani, kikombe ambacho kilijaa hasira yangu, ili kwamba"
# Tazama
Hii ni lahaja inayotumika kuvuta nadhari ya msikilizaji kwa kile kinachosemwa baadaye. "sikiliza"
# kikombe cha kupepesuka
Neno "kikombe" ina maana ya kile kilicho ndani ya kikombe. "kikombe cha divai ambacho huwafanya watu wapepesuke"
# bakuli, ambalo ni kikombe cha hasira yangu
Yahwe anazungumza kuwaadhibu watu kana kwamba aliwalazimisha kunywa kutoka katika bakuli ambalo lilijazwa hasira yake. "bakuli ambalo lilijazwa hasira yangu" au "kikombe ambacho kilijazwa hasira yangu"