sw_tn/isa/49/08.md

24 lines
975 B
Markdown

# Katika kipindi ntakapoamua kuonyesha fadhila yangu nitakujibu, na katika siku ya wokovu nitakusaidia
Vishazi hivi viwili vina maana moja.
# nitakujibu
Hapa "nitakujibu" ina maana ya mtumishi wa Yahwe.
# katika siku ya wokovu
Hapa neno "siku" ina maana ya muda bayana na sio siku ya masaa 24. Neno "wokovu" linaweza kutafsiriwa kama kitenzi. "pale kipindi kitakapokuja kwangu kukuokoa"
# kukupatia kama agano kwa ajili ya watu
Hapa neno "agano" ni mfano wa maneno kwa yule ambaye huanzisha au kupatanisha agano. "kukufanya kuwa mpatanishi wa agano na watu"
# kuijenga tena nchi
Hapa neno "nchi" inawakilisha miji katika nchi ambayo ilikuwa imeangamizwa. "kujenga tena sehemu zilizoharibiwa katika nchi"
# kugawia tena urithi uliotelekezwa
Yahwe anazungumzia nchi kana kwamba ilikuwa urithi ambao watu wa Israeli walipokea kama milki ya milele. Inadokezwa ya kwamba mtumishi atagawa tena nchi kwa watu wa Israeli. "kugawa tena nchi iliyotelekezwa kama urithi wao"