sw_tn/isa/49/05.md

24 lines
1.1 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Mtumishi wa Yahwe anaendelea kuzungumza.
# kwamba Israeli aweze kukusanywa kwake
Sehemu hii ya sentensi ina maana moja na sehemu kabla yake. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kuleta watu wa Israeli kwake mwenyewe"
# Nimeinuliwa katika macho ya Yahwe
Hapa "macho" yanawakilisha mawazo ya Yahwe au fikra. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe ameniinua"
# Mungu wangu amekuwa nguvu yangu
Mungu kumpa mtumishi nguvu inazungumziwa kana kwamba Mungu mwenyewe alikuwa nguvu yake. "Mungu wangu amenipa nguvu" au "Mungu wangu ameniimarisha"
# nitakufanya kuwa mwanga kwa watu wa mataifa
Mtumishi kuleta ujumbe wa Yahwe kwa watu wa mataifa na kuwasaidia kuelewa inazungumziwa kana kwamba Yahwe alimfanya mtumishi mwanga ambao hung'aa katika watu wa mataifa.
# mpaka mwisho wa dunia
Sehemu juu ya dunia ambazo zipo mbali sana zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa sehemu ambapo dunia hufika mwisho. Msemo huu pia huunda neno lenye maana moja na kundi la vitu kumaanisha kila sehemu katikati ya mwisho. "katika sehemu zote za mbali za dunia" au "katika dunia nzima"