sw_tn/isa/42/23.md

24 lines
1.0 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Hapa Isaya anaanza kuzungumza
# Nani kati yenu
Hapa "yenu" ni wingi na ina maana watu wa Israeli.
# Ni nani alimpatia Yakobo kwa mnyanganyi, na Israeli kwa waporaji?
Misemo hii miwili ina maana ya jambo moja. Isaya anatuma hii kama swali la kuongoza ili kusisitiza jibu ambalo atalitoa katika msemo unaofuata. "Nitakuambia ni nani aliwapa watu wa Israeli kwa wanyanganyi na waporaji"
# Je! haikuwa Yahwe ... walikataa kutii?
Isaya anatumia swali hili la balagha kusisitiza ya kwamba Yahwe pekee alikuwa anawajibika kwa hali ya Israeli, na kufafanua sababu ambayo Yahwe alifanya vile. "Hakika alikuwa Yahwe ... walikataa kutii".
# ambaye tumetenda dhambi dhidi yake
Hapa neno "tumetenda" ina maana ya watu wa Israeli na Isaya.
# ambazo katika njia zake walikataa kutembea, na katika sheria yake walikataa kutii
Neno "walikataa" pia ina maana ya watu wa Israeli na Isaya. Misemo miwili ina maana moja. Katika ya kwanza, kutii sheria za Yahwe inazungumziwa kana kwamba ilikuwa kutembea katika njia ambayo Yahwe aliamuru kutembea.