sw_tn/isa/42/14.md

24 lines
844 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Yahwe anaendelea kuzungumza.
# Nimekaa kimya kwa muda mrefu; Nilikuwa nimetulia n kujizuia
Mistari hii miwili inagawana maana ya kufanana. Kutulia kwa Yahwe kunafafanuliwa kama ukimya na utulivi.
# Nilikuwa nimetulia n kujizuia
Misemo hii miwili inagawana jambo moja na hudokeza ya kwamba Yahwe amejizuia kutotenda. "Nimejizuia kutofanya chochote"
# Nitalia kama mwanamke katika uchungu; nitahema na kutweta
Utulivu wa Yahwe kama hodari anayepaza sauti inalinganishwa na mwanamke mwenye mimba anayelia kwa maumivu ya uchungu. Hii inasisitiza tendo la ghafla lisilozuilika baada ya kipindi cha utulivu.
# Nitafanya milima kuwa takataka ... Nitakausha mabwawa
Yahwe anatumia lugha hii ya kisitiari kufafanua nguvu yake kubwa kushinda adui zake.
# mabwawa
Bwawa ni eneo laini, lililo tepe tepe lenye madimbwi ya maji