sw_tn/isa/41/14.md

40 lines
1.6 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.
# Yakobo wewe funza, na nyie watu wa Israeli
Hapa "Yakobo" na "watu wa Israeli" ina maana moja. "nyie watu wa Israeli ambao ni kama funza"
# Yakobo wewe funza
Maana zaweza kuwa 1) ya kwamba ina maana ya mawazo ya mataifa mengine kuhusu watu wa Israeli au 2) ya kwamba hii ina maana ya mawazo ya Israeli wenyewe. Yahwe anazungumziwa umuhimu wao kana kwamba walikuwa funza.
# tamko la Yahwe
Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "tamko" linaelezwa kama kitenzi "tamka" au "kusema kwa dhati". "Yahwe alitamka" au "Yahwe alisema kwa dhati"
# Mtakatifu wa Israeli
Mtakatifu wa Israeli
# Ninakufanya kama chombo cha kupura yenye ncha kali ... utaifanya vilima kuwa kama makapi
Yahwe anazungumzia kuwawezesha Israeli kuwashinda adui zao kana kwamba alikuwa akifanya taifa kuwa chombo cha kupura ambayo itasawazisha milima.
# chombo cha kupura yenye ncha kali
chombo cha kupura ilikuwa ubao wenye uma zenye ncha kali ambazo mtu huvuta juu ya ngano kugawanyisha nafaka kutoka na makapi.
# makali pande mbili
Hii ina maana ya pande za uma ambazo ziliungwa katika chombo cha kupura. Ya kwamba walikuwa "makali pande mbili" ina maana walikuwa na makali sana.
# utapura milima na kuikanyaga
Badala ya kupura nafaka, Israeli atapura milima, ambayo inawakilisha mataifa yenye nguvu ambayo yalikuwa adui wa Israeli. "utapura adui zako na kuwaponda kana kwamba walikuwa nafaka, ingawa wanaonekana kuwa kama milima imara"
# utaifanya vilima kuwa kama makapi
Mstari huu una maana sawa na mstari wa nyuma lakini unawakilisha hatua inayofuata katika njia ya kupura nafaka.