sw_tn/isa/33/05.md

24 lines
1015 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Isaya anazungumzia watu wa Yuda
# Yahwe anainuliwa
"Yahwe ni mkubwa kuliko mtu yeyote yule"
# Ataijaza Sayuni kwa hukumu na haki
Hii inazungumzia Yahwe kutawala Sayuni kwa hukumu na haki yake kana kwamba alikuwa akijaza Sayuni kwa hukumu na haki. "Atatawala Sayuni kwa hukumu na haki"
# Atakuwa uthibiti katika nyakati zako
Hii inazungumzia Yahwe kusababisha watu wake kuwa imara kana kwamba alikuwa uthabiti mwenyewe. Msemo "nyakati zako" una maana ya maisha yao. "Atakufanya salama maisha yako yote"
# wingi wa wokovu, hekima, na maarifa
Maneno ambayo hayapo yanaweza kuongezwa. Pia "wokovu" inaweza kuelezwa kwa kitenzi "okoa". "na atakupatia wingi wa wokovu, hekima, na maarifa" au "atakuokoa na kukupa wingi wa hekima na maarifa"
# hofu ya Yahwe ni hazina yake
Hii inazungumzia kumhofu Yahwe kana kwamba ilikuwa hazina ambayo Yahwe hutoa kwa watu wake. "kumcha Yahwe itakuwa kama hazina yenye thamani ambayo atakupatia wewe" au "kumcha Yahwe itakuwa na thamani kwako kama hazina"