sw_tn/isa/30/27.md

28 lines
1.4 KiB
Markdown

# jina la Yahwe ... kma moto unaoteketeza
Yahwe kuwa na hasira kali inzungumziwa kana kwamba alikuwa moto mkubwa.
# jina la Yahwe linakuja
Hapa "jina" linawakilisha Yahwe. "Yahwe anakuja"
# Midomo yake imejaa ghadhabu, na ulimi wake ni kama moto unaoteketeza
Hapa "midomo" na "ulimi" ni mifano ya maneno ambayo inawakilisha Yahwe akzungumza. Na, Yahwe anazungumza na hasira kubwa na uwezo ambao unazungumziwa kana kwamba ulimi wake ulikuwa moto. "Anapozungumza hasira yake ni kama moto ambao huangamiza kila kitu"
# Pumzi yake ni mbubujiko wa nguvu unaomwagikia
Hii inalinganisha hewa inayotoka mdomoni mwa Yahwe kwa mafuriko kusisitiza nguvu yake ya kuangamiza.
# kuchekecha mataifa kwa chungio la uharibifu
Yahwe kutenganisha watu wa mataifa na kuangamiza watu waovu inazungumziwa kana kwamba Yahwe huweka mataifa katika chungio. Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Yahwe atatenganisha na kuangamiza watu waovu wa mataifa"
# Pumzi yake ni hatamu katika taya wa watu kusababisha wazurure mbali
Yahwe kuwa na nguvu ya kusbabisha mipango ya watu kushindwa au kusababisha waangamizwe inazungumziwa kana kwamba pumzi yake ilikuwa hatamu ambayo huongoza watu nje ya njia sahihi.
# hatamu katika taya za watu
"hatamu" ni chombo ambacho watu huwek juu ya kichwa cha farasi kuiongoza. Hatamu huwa na kipande kidogo kinachoitwa "lijamu" ambayo huwekwa katika mdomo wa farasi. "hatamu juu ya vichwa vya watu" au "lijamu katika taya za watu"