sw_tn/isa/28/17.md

32 lines
1.5 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Yahwe anaendelea kulinganisha kile atakachofanya kwa ajili ya watu wa Yerusalemu kwa mjenzi kuandaa jengo.
# Nitafanya hukumu fimbo ya kupimia, na haki timazi
Yahwe kujaribu kulingana na hukumu yake na haki kuthiibitisha kama watu wana haki inazungumziwa kana kwamba alikuwa mjenzi akitumia vifaa kuthibitisha ya kwamba kitu ni urefu sahihi na usawa wa kamili.
# fimbo ya kupimia
Mjenzi hutumia fimbo ya kupimia kubainisha kama kitu kina urefu sahihi.
# timazi
Mjenzi hutumia fimbo ya kupimia kubainisha kama kitu kipo wima na usawa.
# Mvua ya mawe itaondoa
Yahwe kusababisha kiasi kikubwa cha mvua ya mawe kuanguka inazungumziwa kana kwamba itakuwa mafuriko makubwa. "Mvua za mawe zitaangamiza"
# Mvua ya mawe ... maji ya mafuriko
Maana zaweza kuwa 1) maneno yenye maana sawa yanayowakilisha kitu chochote kwa ujumla ambacho kitasababisha uharibifu au 2) hizi ni sitiari kwa jeshi la adui ambalo Yahwe atalituma kuangamiza watu wa Yerusalemu.
# Mvua ya mawe
Vipande vikubwa vigumu vya barafu ambavyo huanguka kutoka angani
# kimbilio la uongo ... sehemu ya kujificha
Hii inazungumzia kuhusu "uongo" kana kwamba ulikuwa sehemu ambao mtu angeweza kwenda kujificha. Inawakilisha kile viongozi wa Yerusalemu waliamini kuwaweka salama kwa adhabu ya Yahwe. Maana zaweza kuwa 1) viongozi wanaamini katika uongo wao wenyewe ambao wamesema ili kujilinda wenyewe au 2) viongozi wanaamini ya kwamba agano walilofanya na miungu ya uongo ya sehemu ya wafu itawaweka salama au 3) viongozi wanaamini ya kwamba makubaliano na Wamisri yatawaweka salama.