sw_tn/isa/24/17.md

24 lines
973 B
Markdown

# Hofu kuu, shimo, na mtego upo juu yako, wakazi wa dunia
"Nyie watu wa dunia mtapitia hofu kuu, shimo, na mtego"
# shimo, na mtego ... atakamatwa katika mtego
Hapa "shimo" na "mtego" inawakilisha mambo mabaya yote tofauti ambayo yatatokea kwa watu. Watu watatoroka kitu kimoja kibaya lakini watapitia kitu kingine kibaya.
# sauti za hofu kuu
"sauti ya kutisha"
# atakamatwa katika mtego
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "mtego utamkamata"
# Madirisha ya mbinguni yatafunguliwa
Hii inazungumzia kiasi kikubwa cha mvua kunguka kutoka angani kana kwamba Yahwe alifungua dirisha katika anga na kuruhusu maji kumwagika. "Anga itafunguka wazi na mvua nyingi itamwagika"
# misingi ya dunia itatikisika
Neno "msingi" kawaida lina maana ya umbo la mawe ambalo hutoa mhimili kwa jengo kutok kwa chini. Hapa inaelezea umbo la kufanana ambalo lilidhaniwa kushikilia dunia katika sehemu yake. "dunia itatikisika kwa kutisha" au "kutakuwa na tetemeko la kutisha"